send link to app

Quran Tukufu (Koran katika Kiswahili))


4.4 ( 7024 ratings )
Bildung Bücher
Entwickler Tatsiana Shukalovich
Frei

Qurani (Quran) (Quran katika Kiswahili)

Quran (kwa Kiarabu: القرآن) ni kitabu kitukufu cha Uislamu. Quran inatazamiwa na Waislamu kama "Neno la Allah (Mwenyezi Mungu)". Kitabu hiki kwao ni tofauti kabisa na maandiko ya vitabu vya dini nyingine kwa maana hicho kinaaminika kwamba kimeandikwa moja kwa moja na Mwenyezi Mungu, kupitia mtume wake wa mwisho, Muhammad.

Lugha na tafsiri
Imeandikwa na kusomwa kwa lugha ya Kiarabu pekee kwa zaidi ya miaka 1,400.
Kadiri ya Qurani (42:8), Mungu alimuambia Muhammad: "Na namna hivi tumekufunulia Qurani kwa Kiarabu ili uwaonye watu wa Makka na walio pembeni mwake"
Lakini, kwa vile leo Waislamu walio wengi ulimwenguni hawajui Kiarabu, maana halisi ya Quran hutolewa kwa lugha nyingine, hivyo kupelekea wasomaji kuelewa vyema yale maneno ya Kiarabu kwenye Quran yana maana gani. Vitabu hivyo ni kama kamusi kwa ajili ya Quran - hawavisomi hivi kama moja ya sehemu ya Quran tukufu na Waislam, ili kuwa badala ya Quran ya Kiarabu.
Waislamu wengi wanaamini kwamba tafsiri ile siyo ya Quran tukufu na wala siyo ya kweli; ni kopi ya Kiarabu tu iliyotolewa kwenye Quran ya kweli.

Waislamu wanaamini kwamba Quran tukufu mtume Muhammad alipewa na malaika Jibrīl kwenye pango la mlima Hira, kwa kipindi cha zaidi ya miaka ishirini na tatu hadi mauti wake ilipomfikia.
Quran tukufu haikuwa kitabu cha maandiko wakati wa uhai wa mtume Muhammad; iliwekwa kwa mawasiliano ya kimdomo tu. Bimaana, watu walihifadhi kichwani.
Mtume labda hakuwa anajua kusoma wala kuandika, lakini kwa mujibu wa Waislamu, swahaba wake Abu Bekr alikuwa akiandika maandiko yale juu ya kitu fulani wakati huo mtume Muhammad yu hai. Pale Abu Bekr alipokuja kuwa khalifa, ameileta Quran na kuwa kitabu kitakatifu.
Uthman, ambaye ni khalifa wa tatu, ameondoa vipengele ambavyo vilikuwa havihusiani na Quran tukufu.

Elementi, Sura, Mistari, Aya
Kuna sehemu 30 katika Quran, ambayo inafanya kuwa na sura 114. Kila sura ina namba tofauti ya mistari.
Kwa mujibu wa mafunzo ya Kiislam, sura 86 kati ya hizi zimeshuka mjini Makka, sura 24 kati ya hizi zimeshuka mjini Madina.
Miongoni mwa sura zilizoshushwa mjini Medina ni pamoja na Al-Baqara, Al Imran, Al-Anfal, Al-Ahzab, Al-Maida, An-Nisa, Al-Mumtahina, Az-Zalzala, Al-Hadid, Muhammad , Ar-Rad, Ar-Rahman, At-Talaq, Al-Bayyina, Al-Hashr, An-Nasr, An-Nur, Al-Hajj, Al-Munafiqun, Al-Mujadila, Al-Hujraat, At-Tahrim, At-Taghabun, Al-Jumua, As-Saff, Al-Fath, At-Tawba, Al-Insan.

Mahusiano baina Quran na Biblia
Katika Quran tukufu, inasomwa kwamba Wayahudi na Wakristo pia huamini Mungu wa kweli. Dini hizi pamoja na Uislamu huitwa za Abrahamu kwa sababu ya mahusiano haya.
Kuna baadhi ya kurasa za Quran zinazoelezea habari za mambo ya watu wa katika Biblia. Kwa mfano watu wa katika Biblia waliotajwa kwenye Quran ni pamoja na Adamu, Nuhu, Abraham, Lutu, Ismaili, Yakobo, Yosefu, Haruni, Musa, mfalme Daudi, Solomoni, Elisha, Yona, Yobu, Zakaria, Yohane Mbatizaji, Bikira Maria na Yesu.
Hata hivyo, kuna tofauti za muhimu kabisa baina ya Uislamu na toleo la Biblia katika kuelezea habari za aina moja. Kwa mfano, Quran tukufu inaelezea kwamba Yesu Kristo si Mwana wa Mungu, kama jinsi Wakristo wanavyoamini; kwa Waislamu, alikuwa nabii tu, anayeheshimiwa kwa jina la Isa bin Mariamu.
Uislamu unafundisha kwamba haya yanatokea kwa sababu maandiko ya awali ya Biblia yamepotea na hivyo kuna baadhi ya watu wameyabadilisha. Lakini nje ya Quran hakuna uthibitisho wa fundisho hilo.